#Football #Sports

ITALIA KUKOSA KOMBE LA DUNIA KWA MARA YA 3?

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Italia Gennaro Gattuso amethibitisha kwamba wachezaji Gianluca Scamacca na Giacomo Raspadori wataanza mechi ya timu hiyo dhidi ya Moldova leo usiku, ila akasema anahisi kuwa mfumo wa kufuzu kwa kombe la dunia kwa bara Ulaya unahitaji mabadiliko.

Mechi hiyo itaanza saa 22:45 usiku, na ushindi kwa Italia au hata ushindi katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Norway itawaweka tu katika nafasi ya pili, wakidunishwa na Norway kwa ubora wa mabao na hivyo kuwanyima fursa ya kufuzu moja kwa moja kwa kombe la dunia mwaka ujao.

Katika pambano la mwezi Juni, Raspadori na Andrea Cambiaso walifunga mabao katika ushindi wa mabao 2-0

Kocha huyo ameahidi kufanya mageuzi katika kikosi chake.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *