#Local News

MAUAJI UON: DCI YAZIDISHA UCHUNGUZI

Maafisa wa idara ya upelelezi DCI wameimarisha uchunguzi dhidi ya mshukiwa wa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi Jane Atila, Nicholas Mutua, baada ya kuibuka kwamba mshukiwa anahusishwa na dhuluma dhidi ya waathiriwa zaidi.

Kulingana na waathiriwa waliojitokeza hapo jana, mshukiwa aliwavamia na kuwatesa katika msitu wa KEFRI eneo la Kikuyu, akiwalazimisha wampe fedha.

Nayo familia ya Atila imesema mwanao aliuawa baada yao kushindwa kumpa mshukiwa shilingi 2,500 alizodai.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *