NAIROBI, VIUNGA VYAKE KUPATA MVUA
Mvua ya kiwango cha kati hadi kubwa inatarajiwa jijini Nairobi na viunga vyake katika kipindi cha saa 24 zijazo.
Katika taarifa yake iliyotolewa hapo jana kuhusu hali ya anga, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema mvua hiyo itaathiri maeneo ya nyanda za juu zilizo mashariki mwa bonde la ufa ikiwemo Nairobi kufikia leo saa tatu usiku.
Hata hivyo, idara hiyo imesema mengi ya maeneo yatashuhudia vipindi vya anga kavu, huku mvua ikibashiriwa katika baadhi ya maeneo ya nyanda za juu za mashariki na magharibi mwa bonde hilo
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































