MAN UNITED YAPANGA MKATABA MPYA NA KOBBIE MAINOO
Klabu ya Manchester United imepanga kuzungumza kuhusu mkataba wa muda mrefu na kiungo wake Kobbie Mainoo, baada ya kuonyesha mchango mzuri chini ya kocha Michael Carrick.
Mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 2027, ukiwemo chaguo la kuongeza msimu mmoja hadi 2028, lakini United wanataka kuanza mazungumzo ya mkataba mpya mapema mwaka huu ili kumhakikishia huduma ya Mainoo kwa muda mrefu.
United imedokeza kuwa wanaridhishwa na maendeleo yake kikosini na wanasema mchakato wa mazungumzo utahakikisha mchezaji huyo anabaki kuwa sehemu ya timu kuu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































