WALIMU WA JSS WATANGAZA MGOMO
Serikali ina hadi Januari mwaka ujao kuingilia kati na kuepusha mgogoro mwingine katika sekta ya elimu, kufuatia tangazo la mgomo wa walimu wa sekondari msingi JSS shule zitakapofunguliwa.
Walimu hao wapatao 20,000 waliopewa mkataba wa mwaka mmoja mapema mwaka huu, wameapa kulemaza shughuli za masomo hadi watakapopewa mikataba ya ajira ya kudumu.
Wamekosoa agizo la Rais William Ruto kwamba wapewe ajira ya kudumu baada ya kuhudumu kwa miaka 2.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































