BABU OWINO AKANUSHA USHIRIKIANO NA GACHAGUA
Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, amekanusha madai kuwa anatafuta aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, kwa lengo la kushirikiana naye kisiasa, huku akisisitiza kuwa nia yake ni kuchukua uongozi ndani ya chama cha ODM.
Owino amesema lengo lake kuu ni kuvutia kura kutoka kwa jamii zote jijini Nairobi ili kutimiza azma yake ya kuwania ugavana, akiongeza kuwa hatajihusisha na siasa za ukabila kufanikisha ndoto hiyo.
Aidha Owino analenga kuwania kiti cha Ugavana wa Nairobi katika uchaguzi wa 2027, huku kukiwa na madai kwamba anahusishwa na mrengo wa upinzani unaodaiwa kuongozwa na Gachagua pamoja na kinara wa Wiper, Kalonzo Musyoka.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































