#Local News

IEBC YAKANA KUIBA UCHAGUZI

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imepuzilia mbali madai kuhusu uwepo wa udanganyifu katika uchaguzi mdogo wa Magarini kaunti ya Kilifi, ikitoa hakikisho kuwa uchaguzi huo utafanywa kwa njia ya uadilifu na uwazi.

Kupitia taarifa, IEBC imekiri kupokea malalamishi rasmi kutoka kwa kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua kuhusu njama ya wizi wa kura hizo kwa ushirikiano na naibu mwenyekiti wa tume hiyo Fahima Abdalla, ila ikakana madai hayo.

Kwa mujibu wa Gachagua, Abdallah amekuwa akifanya vikao na gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro ili kukisaidia chama cha ODM kuibuka na ushindi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

IEBC YAKANA KUIBA UCHAGUZI

KAMPENI ZA CHAGUZI NDOGO KIKOMO

IEBC YAKANA KUIBA UCHAGUZI

SERIKALI YAAHIDI USALAMA UCHAGUZINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *