WACHEZAJI WA MISRI WAMUUNGA MKONO SALAH
Wachezaji wa timu ya taifa ya Misri wameonyesha kuungana na nahodha wao Mohamed Salah, huku hatma yake ndani ya Liverpool ikibaki na sintofahamu kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco.
Misri ambao ni mabingwa wa Afrika mara saba, wamepangwa Kundi B pamoja na Angola, Afrika Kusini na Zimbabwe
Salah hakujumuishwa kwenye kikosi kilichosafiri Milan kucheza dhidi ya Inter kwenye Ligi ya Mabingwa barani ulaya na ameashiria kuwa huenda asichezee Liverpool tena.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































