#Local News

MURKOMEN ATETEA IDARA YA USALAMA

Huku idara ya usalama ikishutumiwa kutokana na vurugu zilizoshuhudiwa Jumapili kwenye mkutano wa katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna katika eneo la Kitengela, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen ameitetea idara hiyo, akisema haikufahamishwa kuhusu mkutano huo ili kutoa ulinzi kwa waliohudhuria.

Kwenye mkutano katika kaunti ya Nakuru, Murkomen ameonya kuhusu ongezeko la visa vya uchochezi wa kisiasa, akiwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kutuliza joto la kisiasa linalopanda nchini.Naye jaji mkuu wa zamani David Maraga, ameikosoa idara hiyo kwa madai ya kutumia nguvu kupita kiasi katika mikutano ya kisiasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MURKOMEN ATETEA IDARA YA USALAMA

VIONGOZI WA ODM WAMKOSOA KENYATTA 

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *