#Business

IDADI YA WATALII WA CHINA YAFIKIA 100,000 KENYA

Sekta ya utalii nchini imepigwa jeki baada ya taifa hili kushuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watalii kutoka China wanaozuru ili kufurahia vivutio vyake vya kuvutia, vikiwemo wanyamapori na fukwe za mchanga. June Chepkemei, afisa mkuu mtendaji wa Bodi ya Utalii, amesema kwamba mawasiliano yaliyolengwa kwa wasafiri wa China yamezaa matunda, na kuleta uhai katika sekta ya ukarimu ya nchi hii ya Afrika Mashariki.

Idadi ya watalii wa China waliotembelea Kenya mwezi Februari imeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na sikukuu ya Tamasha la Masika ya Uchina, amesema, akibainisha kuwa wengi wa watalii hao walivutiwa na wanyamapori na tamaduni za kiasili.

Kulingana na Chepkemei, Kenya ina bidhaa mbalimbali za utalii ili kuvutia wageni wa Uchina, kuonyesha vyakula vya ndani na aina halisi za burudani. Na kutaja kuwa ili kuendeleza ukuaji wa idadi ya wageni wa Kichina nchini Kenya, Chepkemei amesema waongoza watalii wa ndani wamekubali lugha ya Kichina ili kuwezesha mawasiliano na burudani au wageni wa biashara kutoka taifa la Asia.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *