ODM YAJIANDAA BILA ODINGA
Kamati kuu ya usimamizi wa chama cha ODM imeratibu kikao maalum hii leo kujadili mustakabali wa chama hicho kufuatia kifo cha aliyekuwa kinara wake Raila Odinga.
Mkutano huo utakaongozwa na kaimu kinara wa chama hicho Oburu Odinga, utafanyika katika makao makuu ya Orange House jijini Nairobi.
Inatarajiwa kwamba wajumbe wa kitaifa wa ODM watamwidhinisha Oburu kuwa kinara rasmi, baada ya wajumbe wa Nyanza tayari kumwidhinisha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































