DROO YA FA RAUNDI YA 3
Droo ya kipute cha FA imekamilika huku klabu za Manchester City, Manchester United, Arsenal na Liverpool zikiwa miongoni mwa klabu 20 za ligi kuu ya Uingereza zilizowafahamu wapinzani wao kwenye raundi ya 3 ambayo pia itazijumuisha klabu 24 za ligi ya Championship.
Klabu hizo zitajiunga na klabu nyingine za ligi za chini kama Macclesfield, Weston-Super-Mare na Boreham Wood ambazo zimefuzu raundi hiyo.
Boreham watachuana na mshindi kati ya Brackley Town na Burton Albion, huku Macclesfield wakipambana na bingwa mtetezi Crystal Palace.
Chelsea watamenyana na majirani zao wa London Charlton Athletic, nao Arsenal wakiratibiwa kupambana na Portsmouth ugenini.
Manchester City, United na Liverpool watakuwa nyumbani kwa mechi zao, City wakiikaribisha Exeter, United waialike Brighton katika pambano la timu za ligi kuu, ilivyo kwa Tottenham na Aston Villa nao Liverpool wakilenga kuweka kando masaibu yao dhidi ya Barsely.
Mechi hizo zitachezwa Januari 10 mwaka ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































