AMORIM: UNITED KUIMARIKA ZAIDI SIKU ZIJAZO
Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema kikosi chake kimeimarika pakubwa baada
ya kurejea katika kinyang’anyiro cha kufuzu Ligi ya Mabingwa kufuatia ushindi wa 4–1 dhidi ya
Wolves.
United ilirekebisha makosa ya sare ya kuwakatisha tamaa dhidi ya West Ham wiki iliyopita,
ikiongozwa na nahodha Bruno Fernandes aliyefunga mabao mawili katika mchezo uliochezwa
Molineux.
Mabao mengine ya United yalifungwa na Bryan Mbeumo na Mason Mount, ushindi ambao Amorim
amesema unadhihirisha mwelekeo mzuri wa kikosi hicho kuelekea hatua ya mwisho ya msimu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































