RATIBA YA IEBC KUELEKEA 2027
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC iko mbioni kufanikisha masuala muhimu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, ikiwemo kuhakikisha kuwa mtandao wa kupeperusha matokeo ya uchaguzi unafanya kazi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kuweka wazi ratiba ya kuelekea kwenye uchaguzi huo, mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amesema tume hiyo imetoa kipaumbele kwa maandalizi ya mapema ya teknolojia ya uchaguzi, katika juhudi za kuzima hofu ya mrengo wa upinzani unaosema hautashiriki uchaguzi iwapo teknolojia ya kampuni ya Smartmatic itatumiwa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, zoezi la kuwasajili wapiga kura wapya kwa wingi itanywa kati ya tarehe 29 Machi hadi Aprili tarehe 29.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































