GHARAMA YA KUBADILI KENYA IWE SINGAPORE NI SH 5 TR, RUTO
Mpango kabambe wa Rais William Ruto wa kubadilisha Kenya hadi nchi ya kwanza ulimwenguni na kupigiwa mfano kama vile nchi za Singapore, Japan, Korea Kusini na Malaysia, utahitaji angalau Ksh.5 trilioni.
Akizungumza wakati wa Hotuba ya Hali ya taifa Bungeni, Rais Ruto amefichua kuwa utawala wake utaweka vipaumbele vinne vya kugeuza mpango huo kuwa ukweli ambayo ni Pamoja na kuwekeza kwa wananchi, kubadilisha uchumi, kuzalisha nishati ya ziada na kubadilisha sekta ya uchukuzi na usafirishaji.
Katika nguzo ya kwanza, Mkuu wan chi amebainisha kuwa serikali haina budi kuwekeza kwa wananchi kupitia elimu, ujuzi, mafunzo ya kisayansi na ubunifu. Rais ruto aidha amebainisha kuwa utawala wake tayari umeweka msingi kupitia mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, kama vile kuongeza bajeti kutoka Ksh.490 bilioni hadi Ksh.700 bilioni katika miaka minne na kuongeza kozi za STEM ili kuimarisha uvumbuzi na kukuza utafiti.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































