3K FC YALENGA KUENDELEZA REKODI NZURI DHIDI YA GUCHA STARS
Timu ya 3K FC inayoshiriki Ligi ya Daraja la Kwanza (NSL) inatarajiwa
kuendeleza kiwango chake kizuri inapowakaribisha Gucha Stars katika
mzunguko wa tisa wa ligi hiyo kwenye uwanja wa Moi Stadium kaunti
ya Embu
Kikosi hicho kutoka Embu kimeonyesha maboresho makubwa
ukilinganisha na msimu uliopita na kwa sasa kinashikilia nafasi ya tatu
kwenye msimamo kwa alama 15 baada ya mechi nane.
Akizungumza kuelekea mchuano huo, kocha mkuu Francis Chege
amesema anaamini kikosi chake kina uwezo wa kupata ushindi
mwingine muhimu kwenye uwanja wao wa nyumbani, akieleza kuwa
wachezaji wako tayari kupambana.
Hata hivyo, alikiri kutarajia mechi ngumu dhidi ya Gucha Stars, timu
ambayo aliitaja kuwa na wachezaji wenye uzoefu na wanaojua
kupambana.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































