#Football #Sports

HOMEBOYZ WASHINDWA KUREJEA ‘NYUMBANI’

Klabu ya Kakamega Homeboyz ilipoteza nafasi ya kurejea kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya soka KPL kufuatia kichapo cha mabao 2-0 mikononi mwa Mathare United wikendi hii, na kuwapa Gor Mahia nafasi ya kuendelea kuongoza licha yao kukosa kuwa na mechi wikendi hii.

Homeboyz ambao wamecheza mechi 9 kufikia sasa, wana pointi 15 katika nafasi ya 2, pointi moja nyuma ya Gor ambao wamecheza mechi 7, AFC Leopards katika nafasi ya 3 kwa pointi 13 baada ya mechi 8.

Katika matokeo mengine, bingwa mtetezi Police FC alimzima bingwa wa zamani Tusker FC kwa kibano cha mabao 2-1, huku Bandari FC wakiandikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sofapaka.

Posta Rangers walitoa sare ya bao 1 dhidi ya Mara Sugar huku KCB FC na Bidco United wakiumiza nyasi bila sababu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HOMEBOYZ WASHINDWA KUREJEA ‘NYUMBANI’

KENYA KUJIOKOA KWENYE DEAFLYMPICS

HOMEBOYZ WASHINDWA KUREJEA ‘NYUMBANI’

KOMBE LA DUNIA: DR CONGO YAWEKA HAI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *