RUTO KUELEKEA ETHIOPIA MKUTANO WA AU
Rais William Ruto ataondoka kuelekea Addis Ababa, Ethiopia, kwa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika.
Mada kuu ya mkutano huo ni kujenga mifumo thabiti ya elimu kwa ajili ya rasilimali watu ya karne ya 21 barani Afrika.
Rais Ruto atazungumzia kuhusu ukosefu wa usawa wa elimu ambao umewaacha watoto milioni 98 barani Afrika bila fursa ya kwenda shule huku pia akitoa ripoti kuhusu hatua ambazo bara limepiga katika kupunguza mgogoro wa tabianchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































