USHAURI WA NATEMBEYA KWA IEBC
Wakati uo huo, gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, ametoa changamoto kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutumia uchaguzi mkuu ujao kurejesha imani ya wakenya, kwa kuhakikisha uwazi uhuru na haki katika matokeo hasa ya urais.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, gavana huyo amesema kuwa wakenya wamekosa imani kwenye tume hiyo kutokana na jinsi imekuwa ikiendesha chaguzi.
Amewataka wakenya kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































