#Local News

WABUNGE, MASENETA KAZINI LEO

Maseneta na wabunge hatimaye wanarejelea vikao vyao hii leo bungeni baada ya likizo ya miezi 2, spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula akiratibiwa kukutana na viongozi wa bunge saa nne asubuhi kupanga namna vikao hivyo vitaendeshwa.

Miongoni mwa masuala yanayotarajiwa kupewa kipaumbele kwenye mijadala ya bunge ni mpango wa serikali kuuza asilimia 15 za hisa za kampuni ya mawasiliano ya Safaricom, ambao uko katika hatua ya ukusanyaji wa maoni ya wakenya kuuhusu.

Aidha, suala la kupunguza ushuru unaotozwa kwenye mishahara ya wafanyakazi linatarajiwa kujadiliwa, mbali na uwezekano wa kufanya mabadiliko ya uongozi bungeni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WABUNGE, MASENETA KAZINI LEO

MIKAKATI YA MISAADA YA UKAME

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *