#Football #Sports

VIHIGA QUEENS WALENGA KUREJELEA UBINGWA KWPL

Meneja wa klabu ya Vihiga Queens inayosakata ligi kuu ya wanawake nchini KWPL Boniface Nyamunyamuh, anasema kikosi chake kinalenga kurejelea ubingwa wa taji hilo msimu huu na kwamba atafanya kila awezalo kuhakikisha ndoto hiyo inatimia.

Nyamunyamuh aliyewaongoza vipusa hao kumaliza katika nafasi ya 3 msimu jana kwa alama 41, zikiwa alama 8 nyuma ya mabingwa Police Bullets, anasema ukubwa wa kikosi chake na ujio wa wachezaji wapya utakuwa nguzo katika kufanikisha hilo.

Mabingwa hao mara 4 wameanza msimu kwa kishindo, wakiinyuga Bungoma Queens mabao 3-0 katika mechi ya ufunguzi, ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kibera Soccer Ladies kabla ya ushindi mwingine wa mabao 6-0 dhidi ya Kisped wa Kisumu Jumapili iliyopita.

Ushindi huo mara 3 mfululizo umewaweka kileleni kwa jedwali la ligi kwa pointi 9 sawa na Police Bullets wanaodunishwa kwa ubora wa mabao.

Ulinzi Starlets, Trinity Starlets na Kayole Starlets wanafunga 5 bora.

Vipusa hao wa Vihiga wamewasajili wachezaji 8 msimu huu kuimarisha kikosi chao, akiwemo mshambulizi Irene Madalina kutoka Yanga ya Tanzania, kiungo Noel Shilachilo na beki Georgina Mulati kutoka Fountain Gate Princess ya Tanzania. 

Wengine ni raia 3 wa Uganda amba oni kiungo Anita Namata kutoka Kampala Queens, beki Sharifa Kabiite kutoka Rines SS WFC na kiungo Damaris Matama aliyesajiliwa kutoka Kampala Queens.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

VIHIGA QUEENS WALENGA KUREJELEA UBINGWA KWPL

WANASIASA, WAFUASI WAONYWA KABUCHAI

VIHIGA QUEENS WALENGA KUREJELEA UBINGWA KWPL

LIVERPOOL WAWAWEKA LOS BLANCOS GIZANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *