SLOT ASISITIZA ATAINUSURU LIVERPOOL
Meneja wa klabu ya Liverpool Arne Slot ameapa kuendelea kupambana,akisema mazungumzo kati yake na wamiliki wa Liverpool haijabadilika licha ya matokeo duni yanayoendelea kuandikishwa na klabu hiyo.
Mabingwa hao wa EPL walipepetwa magoli 4-1 na PSV Eindhoven kwenye dimba la klabu bingwa bara Ulaya Jumatano, kikiwa kichapo chao cha 9 katika mechi 12 zilizopita.
Hatua hiyo iliwafanya mashabiki kuondoka uwanjani kwa wingi mechi hiyo ilipokuwa ikielekea kutamatika.
Wikendi hii, wekundu hao wa Anfield wanasafiri kukabiliana na nyundo ya West Ham, wakilenga kujifufua baada ya kuzamishwa katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi ya kwanza.
Hata hivyo, Slot aliyewaongoza Liverpool kutwaa EPL kwenye msimu wake wa kwanza msimu jana, alisema baada ya kichapo hicho kwamba kazi yake iko salama.
Slot alikubali kudorora kwa fomu ya klabu yake, ila akasisitiza kuwa hahisi kuwa anaangushwa na wachezaji wake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































