#Local News

ODM YAZINDUA ZIARA ZA KAUNTI

Chama cha ODM, kimetangaza kuanza kwa ziara zake za kaunti chini ya kaulimbiu ya Linda Ground, zitakazoanza Jumamosi, Januari 17, 2026.

Tangazo hilo lilitolewa kupitia bango rasmi la chama, likieleza ratiba na maeneo ya ziara hiyo huku Kituo cha kwanza cha ziara hiyo kikiwa Malaba, Kaunti ya Busia, tarehe 17 Januari, kabla ya kufuatiwa na kituo cha pili katika mji wa Kakamega tarehe 18 Januari.

Ziara hiyo ya mwisho wa wiki inatarajiwa kuwashirikisha wafuasi wa chama, viongozi wa jamii pamoja na wakazi, huku ODM ikilenga kuimarisha uwepo wake mashinani katika eneo la Magharibi mwa Kenya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

ODM YAZINDUA ZIARA ZA KAUNTI

WAKO WAPI WANAFUNZI WA GRADE 10?

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *