#Sports

UBABE WA HANDIBOLI WATARAJIWA WIKENDI

Fataki zinatarajiwa katika ulingo wa mchezo wa handiboli nchini Jumapili hii wakati mabingwa watetezi wa ligi ya shirikisho la handiboli kwa wanaume National Cereals Board NCPB, watalenga kuzuia uharibifu wa nafaka yao kutoka kwa risasi za mahasimu wao wa jadi Ulinzi ugani Nyayo.

Kocha mkuu wa NCPB Bryan Mathews ameelezea matumaini ya kuendeleza ubabe wao dhidi ya wanajeshi hao.

Msimu jana, wananafaka hao waliwalaza Ulinzi katika mizunguko yote miwili, na watalenga kuendeleza kichapo msimu huu.

Hata hivyo, Mathews ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya handiboli, amesema watachukulia kila mechi kuwa fainali wanapojiandaa kutetea taji lao katika ligi yenye mwonekano mpya ambapo kila timu itamenyana na mwenzake mara 2.

Wakati uo huo, mwenzake wa Ulinzi Victor Ochieng, amesema wamejiandaa kisawasawa na kuboresha udhaifu wao, na anaamini kuwa huu ndio msimu wao wa mwamko mpya.

Kabla ya pambano hilo, timu hizo zina mechi tofauti hapo kesho, NCPB wakichuana na Kenyatta University nao Ulinzi wakilenga kuvuna point izote dhidi ya Desert Scorpions.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UBABE WA HANDIBOLI WATARAJIWA WIKENDI

AFUENI YA SARATANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *