UPINZANI: IDARA YA POLISI IMETEKWA NA MUKROMEN, OMOLLO
Viongozi wa muungano wa upinzani wameibua madai kwamba serikali ya Rais William Ruto inatumia idara ya usalama kuwahangaisha wakosoaji wake, kwa lengo la kuibua hofu miongoni mwa wafuasi wa wakosoaji.
Viongozi hao akiwemo Rigathi Gachagua wa DCP, Kalonzo Musyoka wa Wiper, na Eugene Wamalwa wa DAP-K, wamedai idara ya polisi inatumika kuendeleza uhuni, wakimtaka Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja kujiuzulu iwapo idara hiyo imetekwa na wizara ya masuala ya usalama chini ya Waziri Kipchumba Murkomen na katibu wake mkuu Raymond Omollo.
Musyoka amesema wanakusanya ushahidi kwa lengo la kuishtaki serikali katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC kuhusiana na ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































