CITY THUNDER YANGURUMA NJIANI KUELEKEA BAL ELITE 16
Klabu ya Nairobi City Thunder ilinguruma na kuibwaga Namuwongo Blazers ya Uganda 89-62 katika mechi ya ufunguzi ya mashindano ya Basketball Africa League yaani BAL Elite 16 kanda ya Mashariki ugani Kasarani hapo jana.
Klabu hiyo ya hapa nchini ilidhibiti mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho, ikidhihirisha ukubwa wa kikosi chake, nguvu na ubora katika ufungaji.
Thunder ilianza kwa kishindo, ikidhibiti kasi na kuiadhibu Blazers kwa utepetevu katika safu ya ulinzi.
Kabla ya mchuano huo, pambano la kupamba moto lilishuhudiwa baina ya Dar City Basketball na Matero Magic, Dar wakiwalima Magic 85-78 kwenye pambano lilisheheni kasi ya aina yake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































