KINYANG’ANYIRO CHA EPL CHASHIKA KASI
Manchester City walitia joto kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL, baada ya kupata ushindi kwa ulaini wa mabao 3-30 nyumbani dhidi ya Fulham, na kupunguza pengo la pointi kati yao na viongozi Arsenal.
Arsenal, ambao katika misimu 2, 3 iliyopita waliyumba na kupoteza uongozi kutokana na shinikizo la City, wataingia uwanjani leo ugenini dhidi ya Brentford, wakilenga mambo 2- mwanzo kurejesha uongozi wa pointi 6, na pili kuwahakikishia wafuasi wake kwamba hawatayumba na kuwaweka katika hali ya kungoja ‘next season’.
Mabao 3 ya City katika muda wa dakika 15 katika kipindi cha kwanza yalitosha kuwaadhibu Fulham, wing’a Antoine Semenyo akiwaweka City kifua mbele kabla ya Nico O’Reilly kufunga la pili, kisha Erling Haaland akatia msumari wa mwisho kwenye sanduku la The Cottagers.
Kwa sasa Arsenal wangali kileleni kwa pointi 56, City wakifuata kwa karibu na pointi 53.
Liverpool waliopata ushindi wa 1-0 dhidi ya Sunderland baada ya kufungiwa na beki Virgil Van Dijk, wanashikilia nafasi ya 6 kwa pointi 42, ingawa huenda wakapitwa na Brentford iwapo wataandikisha ushindi dhidi ya Arsenal.
Wakati uo huo, Nottingham Forest wamemfuta kazi kocha wao Sean Dyche baada ya kuandikisha sare dhidi ya Wolves jana usiku.
Haya yanajiri siku moja baada ya Tottenham kumtimua kocha wao Frank Thomas kutokana na msururu wa matokeo duni, ya hivi punde yakiwa kichapo nyumbani walipoialika Newcastle.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































