#Sports #Swiming

KENYA AQUATICS KUFANYA KAMBI YA MAZOEZI YA JUU APRILI

Shirikisho la kuogelea nchini, Kenya Aquatics, litaandaa kambi ya mazoezi ya kiwango cha juu mwezi Aprili kwa lengo la kuandaa kizazi kijacho cha mabingwa wa kuogelea.

Kambi hiyo itawakutanisha zaidi ya waogeleaji vijana 100 wenye vipaji kutoka maeneo mbalimbali ya nchi, wenye umri kati ya miaka tisa hadi 17, wakati wa likizo ya shule.Mkurugenzi wa kiufundi wa Kenya Aquatics, Omar Omari, alisema kipindi cha likizo ni fursa mwafaka ya kuwakusanya waogeleaji bora wa vijana chini ya paa moja na kuwapa mafunzo ya kitaalamu na msaada mahsusi wa kukuza vipaji vyao

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *