TUCHEL AMPA ONYO BELLINGHAM KUHUSU NAFASI YAKE KATIKAKIKOSI CHA ENGLAND
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Thomas Tuchel, amemuonya
kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham, kwamba atapaswa
kupigania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Uingereza
kuelekea Kombe la Dunia.
Bellingham amerudi kwenye kikosi cha Tuchel kwa michezo ya
mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na Albania wiki hii,
baada ya kukosa mwito mwezi Oktoba kutokana na jeraha la bega.
Katika kipindi hicho, Morgan Rogers wa Aston Villa ameng’ara katika
nafasi ya namba 10, akitoa ushindani mkubwa kwa Bellingham.
Tuchel amesema kwamba atakuwa na maamuzi magumu kuhusu nani
ataanza katika kikosi cha kwanza wakati England wakijiandaa kwa
Kombe la Dunia 2026 litakalofanyika Marekani, Kanada na Mexico.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































