PVK YAPINGA MSWADA WA MAKANISA 2024
Muungano wa Pentecostal Voice of Kenya PVK umepinga mswada wa kudhibiti mashirika ya kidini wa mwaka 2024 uliopendekezwa na serikali, ambao kwa sasa uko katika hatua ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi.
Chini ya mwenyekiti wake Apostle Peter Manyuru ambaye pia ni kiongozi wa kanisa la JTM, muungano huo umeibua hofu kuhusiana na vipengee kadhaa kwenye mswada huo, hasa pendekezo la kubuniwa kwa tume ya kuangazia masuala ya kidini, itakayopewa jukumu la kubuni sera na kutoa uangalizi kwa shughuli za makanisa.
Kulingana na PVK, mswada huo utakandamiza uhuru wa makanisa iwapo utapitishwa na kuwa sheria.
Aidha, Apostle Manyuru ametoa wito kwa Rais William Ruto kutoa msimamo wake kuhusu mswada huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































