HARAMBEE STARLETS WAJIANDAA KWA WAFCON 2026
Timu ya taifa ya wanawake ya Kenya, Harambee Starlets, inaongeza mwendo wa mazoezi huku michuano ya WAFCON ikikaribia, itakayofanyika nchini Morocco.
Kocha mkuu Beldine Odemba amesisitiza kuwa changamoto hazitatatiza maandalizi, licha ya timu kushindwa kucheza mechi za kirafiki nyumbani lakini Odemba amesema kuwa lengo ni kuboresha rekodi ya timu kutoka mwaka wa 2016 ilipoondolewa kwenye hatua ya makundi.
Mlinzi mwenye uzoefu, Dorcas Shikobe, ameonyesha imani kubwa katika kikosi hiki, akibainisha kwamba wachezaji wa kizazi kipya wako tayari kuchukua nafasi kikamilifu na kuendeleza ushindi wa timu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































