#Local News

KHRC YATHIBITISHA KUKAMATWA KWA WATETEZI WA HAKI SITA NAIROBI

Tume ya Haki za Binadamu Kenya, KHRC, imethibitisha kukamatwa kwa watetezi sita wa haki za binadamu waliokuwa wakitoa ombi katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi

Kulingana na tume hiyo, Miongoni mwa waliokamatwa ni Frederick Ojiro, Julius Kamau, Vincent Mboya, Lichuma na Shem huku Mwanaharakati mwingine, Geoffrey Mboya, akifafanua kuwa walienda ubalozini kuonyesha mshikamano na wananchi wa Tanzania.

Kundi hilo limekuwa likiitisha uwajibikaji kufuatia madai ya mauaji ya watu wengi nchini Tanzania baada ya uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata, ambapo Samia Suluhu alitangazwa mshindi bila upinzani mkubwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KHRC YATHIBITISHA KUKAMATWA KWA WATETEZI WA HAKI SITA NAIROBI

UPINZANI: IEBC KIBARAKA WA SERIKALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *