WAKENYA WATAHADHARISHWA DHIDI YA BIDHAA GHUSHI
Mamlaka ya kukabiliana na bidhaa ghushi nchini, ACA, imewatahadharisha wakenya dhidi ya kumia bidhaa hizo, ikisema matumizi ya bidhaa hizo yamechangia madhara makubwa kwa uchumi wa taifa.
Katika kikao na wanahabari baada ya kongamano la siku moja na wadau mbali mbali mjini Bungoma, mkurugenzi wa mamlaka hiyo Henry Maina, amesema kuwa Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayokabili tatizo la matumizi ya bidhaa ghushi.
Amesema ACA imefanikiwa kuzuia bidhaa ghushi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8 katika muda wa miaka 15 tangu kubuniwa kwake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































