UPINZANI KUPINGA MATOKEO YA CHAGUZI MAHAKAMANI
Muungano wa upinzani umetangaza kuelekea mahakamani wiki hii kupinga matokeo ya chaguzi ndogo hasa katika maeneo bunge ya Malava na Mbeere North zilizofanyika wiki jana, kwa misingi kwamba kulikuwa na ukiukaji wa sheria wakati wa chaguzi hizo.
Kwa mujibu wa kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, kulikuwa na vurugu, kuwahonga na kuwatisha wapiga kura miongoni mwa visa vingine vya ukiukaji wa sheria za uchaguzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































