NG’ENO, WENGINE 5 KUPEWA BURIANI
Miili ya watu 6 walioangamia kwenye ajali ya ndege kaunti ya Nandi akiwemo mbunge wa Emurua Dikirr kaunti ya Narok Johana Ng’eno, itasafirishwa leo hii kwa ibada ya pamoja katika shule ya msingi ya Emurua Dikirr ambako pia wakazi watapata fursa ya kuitazama kabla ya mazishi hapo kesho.
Ibada ya leo inajiri baada ya nyingine kufanyika hapo jana jijini Nairobi iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Naibu Rais Kithure Kindiki, na waombolezaji wengine.
Ng’eno amekumbukwa kama kiongozi shupavu aliyejitolea kuboresha maisha ya wakazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































