#Local News

MAHAKAMA YAIDHINISHA FAINI ZA PAPO HAPO

Mfumo mpya wa mamlaka ya usalama barabarani, NTSA, kuwatoza faini za papo hapo madereva wanaovunja sheria za trafiki utaendelea kutekelezwa, baada ya mahakama kuu kutupilia mbali kesi iliyokuwa ikiupinga.

Kwa mujibu wa walalamishi wakiongozwa na dereva Kennedy Maingi, mfumo huo unaipa NTSA mamlaka ya kuwanyanyasa madereva barabarani, hoja ambayo NTSA imepinga ikisema mfumo huo unalenga kuleta nidhamu.

Nashon Kondiwa ni mkurugenzi wa mamlaka hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *