#Local News

NPS YATAKA MABILIONI ZA UCHAGUZI

Huku washikadau mbali mbali wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, idara ya polisi imelitaka bunge kuitengea mgao wa shilingi bilioni 21 zaidi ili kufanikisha maandalizi yake, ikiwemo ununuzi wa magari kwa baadhi ya vituo vya polisi.

Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama, Inspekta Mkuu wa polisi Douglas Kanja, amesema kuwa idara hiyo inakabiliwa na upungufu wa maafisa wa polisi 15,000, huku nusu ya vituo vikikosa magari.

Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 2 zimetengewa ununuzi wa vifaa vya mawasiliano.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *