SERIKALI KUIMARISHA UTAFITI NA UBUNIFU VYUONI
Rais William Ruto amesema Serikali inaweka utafiti na ubunifu kuwa nguzo kuu katika mafunzo ya elimu ya juu ili kukuza maarifa na ushindani wa taifa.
Ruto amesema kuanzishwa kwa idara maalum ya serikali ya sayansi, utafiti na ubunifu kunadhihirisha dhamira ya kitaifa ya kuimarisha mafunzo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, (STEM).
Aidha Ruto Amesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha uvumbuzi, kukuza ugunduzi wa kisayansi na kubadilisha mawazo bunifu kuwa biashara zitakazochangia ukuaji wa uchumi na ajira.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































