DROO YA CARABAO
Bingwa mtetezi wa kombe la Carabao Newcastle United watachuana na Fulham katika awamu ya robo fainali ya kombe hilo, huku Arsenal wakiratibiwa kumenyana katika debi ya London na Crystal Palace.
Palace walifuzu robo fainali jana usiku baada ya kuwatandika wanyonge wao Liverpool mabao 3-0 ugani Anfield, na hivyo kuwacharaza mabingwa hao wa Uingereza mara zote 3 ambazo wamkeutana msimu huu.
Nao Newcastle ambao walitawazwa mabingwa msimu jana baada ya kuiadhibu Liverpool kwenye fainali, walifuzu katika awamu yar obo fainali baada ya kuicharaza Tottenham mabao 2-0
Fulham walilazimika kumaliza kwa mikwaju ya penlati kuwabandua Wycombe, huku Arsenal wakiichabanga brighton mabao 2-0.
Pambano kati ya Arsenal na Palace ni marudiano yar obo fainali ya msimu jana, ambapo Gunners walitoka nyuma na kushinda kwa mabao 3-2.
Cardiff City wanaoshiriki League One watakuw wenyeji wa Chelsea waliowashinda Wolves kwa kibano cha mabao 4-3 katika pambano lililoshuhudia Liam Delap kuonyeshwa kadi nyekundu.
Brentford wanasafari kuelekea Etihad kumenyana na Man City kukamilisha robo fainali hiyo.
City walitoka nyuma na kuilaza Swansea City kwa mabao 3-1, huku Brentford wakiwalaza Grimsby mabao 5-0 Jumanne usiku.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































