WAATHIRIWA CHESONGOCH WASALIA KAMBINI
Familia za watu 39 walioangamia kwenye mkasa wa maporomoko ya ardhi katika eneo la Chesongoch kaunti ya Elgeyo Marakwet zinajiandaa kuwazika wapendwa wao huku wengi wa waathiriwa wakiendelea kuishi katika kambi ya muda kufuatia kuharibiwa kwa makazi yao.
Kwa mujibu wa gavana wa kaunti hiyo Wesley Rotich, zaidi ya familia 100 zimehamishiwa katika maeneo yaliyo salama ili kuzuia maafa zaidi.
Maporomoko hayo yaliharibu miundomsingi na vituo muhimu vya kijamii ikiwemo hospitali ya kimisheni ya Chesongoch.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































