MAHAKAMA YAFUTILIA MBALI USAJILI WA MAKURUTU WA POLISI
Mahakama ya uajiri na leba imefutilia mbali zoezi la kuwasajili makurutu wa kujiunga na idara ya polisi lililokuwa limeratibiwa kufanywa hivi karibuni, kwa misingi kwamba zoezi hilo lilikiuka katiba.
Kwenye uamuzi wake, jaji Hellen Wasilwa, ameamuru kwamba tume ya huduma za polisi NPSC haina mamlaka ya kuwaajiri polisi, na kwamba hilo ni jukumu la kikatiba la idara ya polisi NPS.
Uamuzi huo sasa unasitisha zoezi la kuwasajili makurutu 10,000, mbali na kuimarisha uhuru wa kikatiba wa NPS katika usimamizi wa wafanyakazi wake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































