#Football #Sports

AFCON 2025: USIKU WA NUSU FAINALI

Ulimwengu unakutanishwa nchini Morocco leo usiku ambapo semi fainali za kipute cha mataifa bingwa barani Afrika zitachezwa, zikiwaleta Pamoja miamba wa soka barani.

Katika semi fainali ya kwanza, Lions of Teranga wa Senegal watatoa kucha zao dhidi ya Pharaohs wa Misri ambao ni bingwa wa kihistoria mara 7, katika pambano ambalo pia litawakutanisha wachezaji mahiri wa soka Sadio Mane na Mohammed Salah.

Mara ya mwisho kwa Misri kutwaa taji hilo ulikuwa mwaka wa 2010, mwaka mmoja kabla ya Salah kuanza kuichezea Misri, nao Senegal wakitwaa taji hilo mwaka wa 2021.

Senegal wanajivunia nidhamu ya hali ya juu katika safu ya ulinzi na makali kwenye safu ya mbele, wakiwa wamefunga mabao 11 kufikia sasa kwenye dimba hilo, na watajaribiwa na Misri ambao wanaongoza katika kucheza kwenye awamu ya semi fainali, ya leo ikiwa ni semi fainali yao ya 14.

Katika mechi 6 za hivi punde, kila timu imepata ushindi mara 2 huku mechi 2 zikiishia kwenye sare.

Nusu fainali ya pili itawakutanisha wenyeji Atlas Lions wa Morocco dhidi ya Super Eagles wa Nigeria kwa uwindaji wa nafasi katika fainali.

Katika mashindano ya AFCON 2025Nigeria ndio timu yenye mabao mengi zaidi, wakifunga mabao 14, wakionesha nguvu kubwa katika safu ya ushambuliaji.
Kwa upande wa Morocco wanaosaka ubingwa wa AFCON tangu mwaka 1976, wamefika nusu fainali wakiwa wamefungwa bao moja pekee kwenye sare ya bao 1-1 dhidi ya Mali, wakiongoza kwa rekodi bora ya ulinzi katika mashindano haya.

Kwa ujumla, takwimu zinaonesha kwamba mechi za leo huenda zikaamuliwa kwa bao moja tu, au hata mikwaju ya penalti, kama ilivyokuwa mara nyingi katika historia ya mikutano ya timu hizi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

AFCON 2025: USIKU WA NUSU FAINALI

POLICE FC, GOR WASAKA POINTI KPL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *