#Football #Sports

GOR MAHIA WAONYESHA WANGALI MAWINDONI

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya soka nchini, KPL, Gor Mahia, waliweka wazi kwamba wangali katika uwindaji wa taji hilo msimu huu, kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya Mara Sugar na kuwabandua mahasimu wao wa karibu AFC Leopards kutoka uongozi wa ligi hiyo.

K’Ogalo walitamalaki mchezo mwanzoni na kutangaza hatari katika dakika ya 14 kupitia kwa Felix Oluoch, ambaye sasa amefikisha mabao 7 ya ligi msimu huu.

Dakika 14 baadaye, Musa Shariff aliongeza uongozi kabla ya Samuel Kapen kumalizia kazi kunako dakika ya 84 na kuwahakikishia Gor ushindi ambao unawapandisha hadi kileleni kwa pointi 33 sawa na Leopards, ila Gor wana ubora wa mabao.

Wakati uo huo, wenyeji Kakamega Homeboyz waliendeleza rekodi ya matokeo bora, mara hii wakiandikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kariobangi Sharks.

Murang’a Seal walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bidco United, matokeo ya jana yakiacha wazi kinyang’anyiro cha ubingwa na kusalia kwenye ligi.

Police FC waliomtimua kocha wao Dusan Stojanovic, watamenyana na Nairobi United hii leo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GOR MAHIA WAONYESHA WANGALI MAWINDONI

SENEGAL BINGWA AFRIKA

GOR MAHIA WAONYESHA WANGALI MAWINDONI

MMUST RUGBY WAPATA USHINDI ADIMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *