#Local News

UPINZANI WADAI NJAMA YA UDANGANYIFU 2027

Muungano wa upinzani umeibua madai ya kuwepo kwa njama ya kuiba kura kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia kampuni ya Smartmatic iliyotoa huduma za teknolojia kwenye vyombo vya dijitali vya uchaguzi wa mwaka wa 2022, ikitaka kandarasi ya kampuni hiyo ifutiliwe mbali.

Kulingana na viongozi wa upinzani akiwemo kinara wa DCP Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka wa Wiper, Eugene Wamalwa wa DAP-K na aliyekuwa mwanasheria mkuu Justin Muturi, afisa mkuu mtendaji wa tume ya IEBC Marijan Hussein Marijani ni mshirika wa kampuni hiyo, na aliongeza mktaba wa kampuni hiyo kisiri ili kufanikisha wizi huo.

Wameibua madai zaidi kwamba viongozi wa kampuni hiyo wamekuwa na mikutano ya siri nchini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UPINZANI WADAI NJAMA YA UDANGANYIFU 2027

RUTO AWAPOTOSHA WAKENYA, MUSYOKA

UPINZANI WADAI NJAMA YA UDANGANYIFU 2027

DUALE, KUCO WAKOSA MWAFAKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *