#Football #Sports

TIMU 32 KUJUA WAPINZANI WAO CAF, CONFEDERATIONS CUP

Macho yote yameelekezwa nchini Afrika Kusini ambako droo ya kipute cha klabu bingwa barani Afrika na kile cha CAF Confederations Cup kinaandaliwa, klabu 32 zikisubiri kuwafahamu wapinzani wao katika awamu ya makundi.

Droo hiyo inayoandaliwa jijini Johannesburg itaanza saa nane kamili mchana saa za Afrika Kusini, ambazo ni saa saba za mchana Afrika Mashariki.

Mabingwa nara 12 wa klabu bingwa barani Afrika Al Ahly wa Misri, ambao watakuwa katika awamu ya makundi kwa mara ya 23 na Al Hilal wa Sudan ni miongoni mwa timu 16 zinazosubiri kufahamu hatma yao.

Nyingine ni bingwa mara 4 Esperance ya Tunisia, FAR Rabat ya Morocco, JS Kabylie kutoka Algeria, Mamelodi Sundowns wa Afrika Kusini, MC Algiers wa Algeria, Petro de Luanda wa Angola, Power Dynamos wa Zambia, bingwa mtetezi Pyramids wa Misri, na River United wa Nigeria.

Aidha, Morocco wanawakilishwa na RS Berkane, Simba na Yanga wa Tanzania, Stade Malien wa Mali na Sta Eloi Lupopo kutoka DR Coingo.

Katika droo ya CAF Confederations Cup, Nairobi United wa Kenya ni miongoni mwa timu 16 zinazosubiri kwa hamu kufahamu wapinzani wao kwenye awamu ya makundi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

TIMU 32 KUJUA WAPINZANI WAO CAF, CONFEDERATIONS CUP

GOR WALAZIMISHWA KUTOA SARE

TIMU 32 KUJUA WAPINZANI WAO CAF, CONFEDERATIONS CUP

WOLVES WAMNG’ATA KOCHA WAO PEREIRA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *