MUSTAKABALI WA SIFUNA NJIA PANDA
Inasubiriwa kuona mwelekeo wa kisiasa atakaochukua seneta wa Nairobi Edwin Sifuna baada ya kupokonywa wadhifa wa katibu mkuu wa chama cha ODM, ikizingatiwa kuwa nyota ya kisiasa ya mtangulizi wake Ababu Namwamba ilizima, wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wakibashiri kwamba huenda akakigura chama hicho na kujiunga na DCP yake Rigathi Gachagua.
Aidha, wengi wanahoji kuwa huenda shoka hilo likawa mwanzo wa uwanja wa vita vya kisiasa dhidi yake, ikizingatiwa kuwa ametajwa kwenye orodha ya maseneta 4 wanaodaiwa kuitisha hongo kutoka kwa magavana wanaofika mbele ya kamati za seneti.
Awali, Rais William Ruto alidokeza uwezekano wa ODM kumwadhibu Sifuna, naye Gachagua akidai kulikuwa na njama ya kumfurusha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































