SERIKALI KUU, KAUNTI KUSHIRIKIANA KUTOA BASARI
Serikali kuu na zile za kaunti zimetia saini makubaliano kuhusu usambazaji wa basari za kufadhili elimu ya wanafunzi, hatua itakayohakikisha kila mwanafunzi kutoka familia isiyojiweza anafikiwa na ufadhili wa serikali.
Haya ni kulingana na Rais William Ruto, akisisitiza haja ya ushirikiano huo licha ya basari hizo kuwa jukumu la serikali kuu, akisema ushirikiano huo umeidhinishwa na afisi ya mdhibiti wa bajeti ya serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































