VIONGOZI WA ODM WAMKOSOA KENYATTA
Kundi la viongozi kutoka magaharibi mwa nchi limeendeleza shutuma zake dhidi ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kwa madai ya kufadhili mrengo wa ODM unaoongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna, wakisema hatua hiyo itavuruga azma ya eneo hilo kutwaa uongozi wa taifa hili baada ya Rais William Ruto.
Walikuwa wakizungumza katika eneo bunge la Malava, huku mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya chama hicho na UDA hautayumbishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































