MARAGA AIBUA WASIWASI KUHUSU UENDELEVU WA MPANGO WA NYOTA
Aliyekuwa Jaji Mkuu na mgombea wa urais, David Maraga, ameikosoa serikali kuhusu mpango unaoendelea wa NYOTA, akisema kuwa utekelezaji wake unatiliwa shaka.
Maraga amehoji uendelevu wa mpango huo, pamoja na namna shilingi elfu hamsini zinazotolewa kwa wanufaika, akisema huenda zikadhoofisha kufikiwa kwa lengo kuu la mpango huo na kuupa taswira ya kisiasa badala ya maendeleo ya kudumu.
Maraga amesema kuna maswali mengi yanayojitokeza kuhusu jinsi mpango huo unavyotekelezwa, akisisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji ili kuhakikisha unawanufaisha wananchi waliokusudiwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































