NYOTA YA STARLETS KUANGAZA BARANI
Timu ya taifa ya wanawake ya soka Harambee Starlets imefuzu mashindano ya wanawake ya taifa bingwa barani Afrika WAFCON mwaka ujao, baada ya kuwalaza Gambia bao 1:0 hapo jana nchini Senegal na hivyo kuwabwaga kwa jumla ya mabao 4:1.
Baada ya makabiliano katika kipindi cha kwanza bila mafanikio kwa timu zote, Mwanahalima Adam Jereko aliwapa Starlets bao la pekee la mchezo kunako dakika ya 59, na kuihakikishia timu yake tiketi ya kushiriki WAFCON nchini Morocco kuanzia tarehe 17 Machi hadi Aprili 3 mwaka ujao.
Starlets wanajiunga na mataifa ya Algeria, Burkina Faso, Cabo Verde, Ghana, Kenya, Morocco (wenyeji), Nigeria, Malawi, Senegal, South Africa, Tanzania, Zambia.
Cape Verde wameandikisha historia kwa kufuzu mashindano hayo, baada ya timu ya wanaume kufanya kwa kufuzu mashindano ya kombe la dunia mwaka ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































